Baada ya Alikiba kupost ujumbe katika Instagram akidai kuwepo na
mambo yanayoendelea nyuma ya pazia kwenye muziki wake na wengi kutafsiri
amelalamikia kukosa tuzo za Afrima, uongozi wa Diamond aliyeshinda tuzo
tatu umezungumza.Akizungumza katika pindi cha XXL cha Clouds FM, mmoja
kati ya mameneja wa Diamond, Babu Tale alisema walisikitishwa na ujumbe
huo.“Mimi naona asiyekubali kushindwa sio mshindani,” alisema. “Hata
sisi tumeshawahi kuingia kwenye tuzo ambazo na yeye aliongea maneno hayo
alikuwepo na akashinda na hakuna mtu yeyote aliongea sijui mmenunua
tuzo. Mimi nilijua mashabiki ndio wanaongea mpaka msanii anapost kitu
kama kile nikahisi labda kuna mtu amehack akaunti yake. Kwahiyo
nilivyoona vile nikamhukumu sio mshindani,” alisema Tale.
Hata hivyo Tale alisema baada ya kufuta kauli hiyo na kuzungumzia kauli hiyo aligundua huenda alishinikizwa na mashabiki wake.
“
Lakini baadaye baada ya kuona ameongea
vizuri, nikagundua sometimes mtu anaweza kupaniki kwa ajili ya mashabiki
wanaoongea. Lakini mwisho wa siku tunatakiwa tukae meza moja ili
tusukume muziki wetu wa Tanzania. Tukiangalia line up ya muziki wa
Afrika sasa hivi tupo namba mbili, tunakwenda kwenye namba 1,” aliongeza.
Hata huvyo Alikiba aliifuta post hiyo na kudai kuwa hakuandika kwa sababu alikosa tuzo.
Share this
EmoticonEmoticon