Wanawake walio kwenye vikundi kunufaika na mikopo

2:42 PM
Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Wanawake MAGRETH CHACHA
Benki ya wanawake Tanzania- TWB- na kampuni za nguo za NIDA na NAMERA za mjijini DSM, zimeanzisha mikopo nafuu kwa ajili ya wanawake wanaojishughulisha na biashara ya nguo.

Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya Wanawake MAGRETH CHACHA amesema  mikopo hiyo ya muda mfupi itatolewa kwa wanawake walioko kwenye vikundi au mmoja mmoja ambao ni wateja wa benki yake.

Nae mtendaji mkuu wa kampuni za  NIDA na Namera Group HAMZA RAFIQ amesema mikopo hiyo inatolewa kupitia mpango wa kampuni zake za kuboresha viwanda vya ndani vya nguo na kumwinu mwanamke kiuchumi

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »